Umoja wa Ulaya umetahadharisha juu ya njama zinazofanywa na
utawala haramu wa Israel za kutaka kuugawa msikiti mtakatifu wa al-Aqsa
huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Ripoti ya EU iliyochapishwa
kwenye gazeti la The Guardian la Uingereza inasema kuwa, kuendelea
ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi
zilizoghusubiwa za Palestina, kushadidi njama za kuigawa Masjidul Aqsa
pamoja na hujuma za kila mara za Wazayuni dhidi ya Wapalestina
kunahatarisha mustakabali wa Mashariki ya Kati na kwamba hali hiyo
inazidi kuzuia uwezekano wa kuweko kile kinachotajwa kuwa ni ‘suluhu kwa
njia ya mataifa mawili’. Ripoti ya umoja wa Ulaya pia imeashiria
udharura wa kushinikizwa zaidi utawala haramu wa Israel ili ukubali
kurudi kwenye meza ya mazungumzo na Wapalestina bila masharti. Umoja wa
Ulaya umesema Israel inapaswa kuheshimu sheria zote za kimataifa na
kusimamisha mara moja ujenzi zaidi wa vitongoji kwenye ardhi za
Wapalestina.
0 comments:
Post a Comment