Robert Kitur, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mombasa
Inspekta wa Polisi Ibrahim Mohammed
ameuawa kwa kufyatuliwa risasi na watu wenye silaha huko Mombasa, nchini
Kenya. Jeshi la Polisi la Kenya limeeleza kuwa, watu hao waliobeba
silaha hawakumjeruhi mtu yeyote baada ya kutekeleza shambulio hilo.
Robert Kitur Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mombasa amesema kuwa, bila
shaka shambulio la kumuua Inspekta Ibrahim Mohammed lilipangwa na
makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini humo. Hayo yanajiri
katika hali ambayo, tokea serikali ya Kenya ilipoamua kupeleka majeshi
yake nchini Somalia kwa shabaha ya kukabiliana na kundi la al Shabab,
nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kigaidi
na hasa katika Kaunti za Wajir, Mandera na Mombasa.
0 comments:
Post a Comment