KATIKA kupunguza
Madhara ya Kemikali kwa wananchi, Serikali kupitia Wakala wa Mkemia
Mkuu wameanza utoaji wa elimu kwa Madereva na Makondakta wa Magari ya
usafirishaji wa bidhaa hizo ndani na je ya nchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Msimamizi
wa Mifumo ya Ubora na Utafiti wa Kemikali katika Wakala wa Mkemia Mkuu
wa Serikali BEN MALYA, amesema kumekuwa na uelewa mdogo kwa Madereva na
Makondakta juu namna ya kuepusha madhara ya kemikali pale ambapo magari
ya kubeba bidhaa hiyo yanapopata ajali na kemikali kumwagika.
0 comments:
Post a Comment