Msemaji wa Wizara ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa
vikali matamshi ya Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper na kuyataja
kuwa ya kijuba na kipumbavu. Bi. Marzie Afkham amesema madai ya Harper
kwamba Wairani wanaishi chini ya utawala wa kiimla yanaonyesha jinsi
kiongozi huyo alivyo na chuki dhidi ya taifa hili. Kwenye hotuba yake ya
siku ya Jumamosi mbele ya Wairani wanaoishi Canada, Waziri Mkuu Stephen
Harper alidai kwamba Iran inaendeshwa kidikteta na kwamba raia wa nchi
hii hawajui ladha ya demokrasia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Iran amesema Harper anajaribu kutumia madai ya uongo ili kuwashawishi
Wairani wenye uraia wa Canada waunge mkono chama chake kwenye uchaguzi
ujao wa bunge.
Uhusiano wa Iran na Canada ulivurugika zaidi mwaka 2012 baada ya
serikali ya Ottawa kutangaza kuwa imefunga ubalozi wake hapa mjini
Tehran na baadaye kuanza kutoa madai ya uongo na ya kipropaganda dhidi
ya viongozi na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
0 comments:
Post a Comment