Marais wa nchi sita za Afrika watakuwa na mkutano mkubwa jijini
Dar es Salaam, Tanzania hapo kesho ambapo watajadili kwa kina juu ya
kuboresha uwekezaji katika kanda ya Maziwa Makuu. Marais hao ni Joseph
Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Pierre Nkurunziza wa Burundi,
Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa
Kenya na mwenyeji wao wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete. Mkutano huo wa
siku mbili utaambatana na mdahalo baina ya viongozi hao na wadau
mbalimbali katika sekta za biashara na maendeleo. Mjadala wa viongozi
hao utajikita katika umuhimu wa Ukanda wa Kati ambao ni kiungo muhimu
katika ukuaji uchumi wa nchi hizo kwa kuwa husaidia katika uingizaji na
uuzaji wa bidhaa mbalimbali kupitia Tanzania kwa njia za maji, reli na
barabara. Wakati wa mkutano huo, viongozi hao watafanya uzinduzi wa
treni ya mizigo kuelekea Uganda, Rwanda na DRC.
0 comments:
Post a Comment