Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza
safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la
mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake
kutoka 42 kwa wiki hadi 14.
Serikali ya Tanzania inasema huo ndio mkataba wa tangu awali na
kulaumu mamlaka ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia maelewano na
mamlaka ya Tanzania kuhusu jambo hilo.
Tayari baadhi ya wasafiri
wanaotumia ndege za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia shirika
hilo kufuta baadhi ya safari kutoka Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment