Waziri wa Usalama wa Marekani anasema analitia maanani sana tishio la
kundi la Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, kwamba litashambulia maeneo ya
maduka huko Marekani, Canada na Uingereza.
Katika mahojiano
kwenye televisheni, Jeh Johnson alisema pametokea mabadiliko katika
vitisho vya makundi ya wapiganaji Waislamu ambayo sasa yanatoa wito kwa
washabiki wao katika nchi maalumu kufanya mashambulio.
Ulinzi umezidishwa kwenye eneo moja la maduka la Marekani katika jimbo la Minnesota, ambalo lina wakaazi wengi Wasomali
Mwaka
wa 2013, shambulio lilofanywa na Al Shabaab dhidi ya eneo la maduka la
Westgate mjini Nairobi, Kenya, liliuwa watu zaidi ya 60.
0 comments:
Post a Comment