pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Masheikh 50 Waandamana Kwenda Kwa LOWASSA Kumtaka Agombee URAIS 2015.......Wamkabidhi 700,000 Imsaidie Kuchukua Fomu

MASHEKHE wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania Urais 2015. 
  Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia kwenye picha juu) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.

Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
  Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu," alisema.
Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Lowassa amesema "nikifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu."  
Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Mashekhe kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Shekhe Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya. MASHEKHE hao wakiwasili nyumbani hapo kwaajili ya mazungumzo na Lowassa. Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasikiliza viongozi wa msafara huo. Edward Lowassa akizungumza na Mashekhe hao mjini Dodoma. Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlingotini, Kaole, Chalinze, Lugoba, Msata na kwingineko. Duaa ilisomwa na viongozi hao wa dini. Edward Lowassa akiwasindikiza viongozi hao.

0 comments:

Post a Comment