Mwanariadha raia wa Jamaica Usain
Bolt ameshinda kwa urahis katika shindano lake la kwanza mwaka huu huko
barani Ulaya japokuwa ameshindwa kuvunja rekodi yake ya sekunde 20,
kwenye mbio za mita 200 za Golden Spike huko Ostrava Jamhuri ya Czech.
Katika
shindano hilo lililofanyika jana Bolt alitumia sekunde 20.13 ikiwa ya
rekodi yake ya dunia ya sekunde 19.19 akimbwaga mmarekani Isiah Young
"huwezi ridhika kama sivunji sekunde 20" alisema Bolt ambaye anajiandaa
kwa mashindano ya dunia yatakayofanyika Beijing mwezi August. Naye Asafa
Powell ameshinda katika mbio za mita 100 akitumia sekunde 10.04.
0 comments:
Post a Comment