Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa 
limeliokoa kundi la kwanza la takriban wasichana 300 na wanawake 
waliookolewa kutoka kwa kundi la Boko Haram kwenye kambi moja ya 
wakimbizi.
Watu hao wanaripotiwa kusafiri kwa siku tatu kutoka msitu wa Sambisa ulio kaskazini mashariki mwa nchi.
Karibu
 watu 700 wanaripotiwa kuokolewa wiki hii wakati jeshi linapoendelea na 
operesheni ya kulitimua boko haram kutoka kwa ngome zao za mwisho.
Hatma ya wasichana wengine 200 waliotekwa kutoka mji wa Chibok mwaka mmoja uliopita bado haijulikani.
    
    






0 comments:
Post a Comment