pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Watoto 1, 20,000 wamefariki Afrika kwa dawa bandia

Watoto 1, 20,000 wamefariki Afrika kwa dawa bandia
Zaidi ya watoto laki moja na elfu 20 wamepoteza maisha barani Afrika kwa kutumia madawa bandia. Watoto hao walipoteza maisha ndani ya kipindi cha mwaka 2013, kwa kutumia dawa hizo bandia katika nchi za Afrika. Inaelezwa kuwa asilimia 30 ya wahanga hao walikumbwa na maradhi ambayo yanaweza kutibika. Kukosekana Rasilimali Watu (HR), vituo duni vya afya na kupanda kwa bei ya madawa ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha vifo vya watoto hao. Weledi wa mambo wametaja sababu nyingine ya tatizo hilo kuwa ni kukosekana usimamizi mzuri wa serikali za nchi za bara hilo katika kufuatilia madawa bandia na yale ya asili, suala ambalo limetoa mwanya wa kuongezeka kwa soko la madawa hayo.
Bara la Afrika linatajwa kuwa soko zuri kwa ajili ya kuendeshea bidhaa ya madawa bandia suala ambalo limepelekea kuongezeka vifo vya watu hususan watoto wadogo barani humo.

0 comments:

Post a Comment