pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Kenya yakanusha kuuliwa askari wake na ash-Shabab

Kenya yakanusha kuuliwa askari wake na ash-Shabab
Maafisa usalama wa Kenya wamekanusha habari zilizodai kuwa kundi la kigaidi la ash Shabab limeua maafisa wa polisi wa nchi hiyo.
Maafisa hao usalama kutoka eneo la Yumbis, katika Kaunti ya Garissa wamesema kuwa, maafisa wote wa polisi ambao awali walikuwa hawajulikani walipo, wako salama.
Kaimu kamanda wa polisi wa Kaunti ya Garissa, Shadrack Maithya amekanusha habari za kuuawa maafisa 13 wa polisi ya Kenya kwenye shambulio la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa ash Shabab katika eneo hilo. Hata hivyo maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa kwenye tukio hilo la jana jioni.
Maithya ameongeza kwa kusema: Tumewahesabu maafisa hao na kuona wote wapo salama isipokuwa wawili wamejeruhiwa vibaya na wamepelekwa Nairobi kwa matibabu.
Kabla ya hapo msemaji wa kundi la ash Shabab, Abdul'aziz Abu Mus'ab, alikuwa amedai kwamba, shambulizi lililofanywa na kundi hilo katika kijiji cha Yumbis, limeua askari polisi wasiopungua 25 wa Kenya. Hata hivyo madai hayo yamekanushwa vikali na maafisa usalama wa Kenya.

0 comments:

Post a Comment