Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran amesema kuwa
Tehran inatuma misaada ya kibinadamu huko Yemen kupitia nchi nyingine za
pambizoni mwa Ghuba ya Uajemi khususan Oman. Ali Asghar Ahmadi amesema
kuwa hatua ya Saudi Arabia ya kuzizuia ndege za Iran zilizobeba misaada
ya kibinadamu kutua katika uwanja wa ndege wa San'aa mji mkuu wa nchi
hiyo ni kitendo kisicho cha kibinadamu na kinachokinzana na sheria za
kimataifa. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesema kuwa, pamoja na kuweko vizuizi hivyo, lakini
jumuiya hiyo hadi sasa imeweza kuwatumia wananchi wa Yemen shehena tatu
za bidhaa muhimu za mahitajio kupitia taasisi moja ya misaada ya
kibinadamu ya nchini Oman. Ahmadi amesema, anataraji kuwa misaada hiyo
ambayo inajumuisha bidhaa za chakula, madawa na suhula za kitiba,
itawawafikia wananchi wa Yemen hivi karibuni. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Hilali Nyekundu ya Iran amesema kuwa taasisi hiyo iko imejiandaa pia
kutuma misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa zilizala huko Nepal
0 comments:
Post a Comment