Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na madola sita makubwa duniani
yanayounda kundi la 5+1 yamefikia makubaliano muhimu na ya kihistoria
kuhusiana na miradi ya nyuklia ya Iran. Kwa mujibu wa makubaliano hayo
Iran itaondolewa vikwazo vyote ilivyokuwa imewekewa. Matini ya
makubaliano hayo inasema kuwa, vikwazo vyote vya kifedha, kiuchumi,
kibenki, mafuta, gesi, petrokemikali, kibiashara, bima na usafiri na
uchukuzi ilivyokuwa imewekewa Iran vitaondolewa baada ya jambo hilo
kupasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Aidha marufuku
iliyokuwa imewekewa Iran ya kununua ndege za abiria nayo imeondolewa.
Taarifa zaidi kuhusiana na makubaliano hayo itakujieni katika matangazo
yetu ya leo usiku.
0 comments:
Post a Comment