Mjumbe wa harakati ya wananchi ya Answarullah nchini Yemen,
ameituhumu Saudia kwa kutumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa
dhidi ya raia wa nchi hiyo. Ahmad Hashim aliyasema hayo jana Jumapili
alipokuwa akizungumza na Shirika la Habari la Fars News na kuongeza
kuwa, licha ya Umoja wa Mataifa kutangaza kusimamishwa vita nchini
Yemen, lakini Saudia na waitifaki wake wameendelea kuwashambulia raia wa
Yemen kwa silaha zilizopigwa marufuku kimataifa. Hashim ameongeza kuwa,
baadhi ya nchi za Magharibi hususan Marekani zinaunga mkono mashambulio
hayo ya Saudia nchini Yemen na zinashirikiana na utawala huo wa kifalme
wa ukoo wa Aal Saud katika kutenda jinai hizo. Kiongozi huyo wa
harakati ya Kiislamu ya Answarullah, amesisitiza kuwa, utawala wa Aal
Saud unafanya jinai hizo kwa makusudi mbele ya kimya cha jamii ya
kimataifa huku ukikanyaga waziwazi sheria za kimataifa. Ijumaa
iliyopita, Umoja wa Mataifa ulitangaza kusitishwa vita kuanzia siku hiyo
hadi mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani kwa lengo la kufikisha misaada ya
dharura kwa wahanga wa mashambulizi hayo nchini Yemen, hata hiyo Saudia
ilikengeuka usitishaji vita huo, saa chache baada ya kutangazwa ikidai
kuwa haikujua kuwa kuna usitishaji huo wa vita na wala haikuombwa
kufanya hivyo na kibaraka wake, Mansour Hadi.
0 comments:
Post a Comment