Zaidi ya watu 84 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kaskazini mwa Ufaransa.
Lori lililokuwa likienda mwendo wa kasi lilijipenyeza katika
mkusanyiko wa watu waliokuwa wakishiriki maonesho ya fataki kuadhimisha
siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huandamana na shamra shamra kila
mwaka. Polisi walifanikiwa kumuua dereva wa lori hilo baada ya kujiri
majibizano ya risasi yaliyochukua muda mrefu kwenye tukio hilo. Kamanda
wa polisi wa mji wa Nice amekielezea kitendo cha dereva huyo kuwa cha
kigaidi na amewataka wananchi kuchukua tahadhari. Kundi la Daesh
limekiri kuhusika na shambulio hilo lililotokea nchini humo wakati wa
sherehe za maadhimisho ya Siku ya Bastille. Rais François Hollande wa
Ufaransa, sanjari na kulaani shambulizi hilo, amedai kuwa, nchi yake
itaendeleza mashambulizi dhidi ya wanachama wa kundi hilo, nchini Syria.
Inafaa kuashiria hapa kwamba, Ufaransa ni moja ya nchi waungaji mkono
kwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini Syria kwa lengo la
kutaka kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa
nchi hiyo
0 comments:
Post a Comment