Sambamba na kutimia mwaka mmoja tangu
kufikiwa makubaliano ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
kundi la 5+1, baraza la wawakilishi nchini Marekani, limepasisha vikwazo
vipya dhidi ya taifa hili.
Jana baraza la wawakilishi nchini Marekani ambalo linaundwa na
silimia kubwa ya wawakilishi kutoka mrengo wa chama cha Republican,
lilipitisha mpango wa vingee viwili wa vikwazo hivyo kwa kupigiwa kura
ya ndio na wajumbe 246 kati ya 179 waliopinga mpango huo. Wawakilishi wa
Marekani pia walipitisha kwa kura 246 kati ya 181 mpango wa kupiga
marufuku Iran kunufaika na mfumo wa kifedha wa Marekani na pia sarafu
ya dola katika miamala yake ya kigeni. Kabla ya hapo pia yaani siku ya
Jumatano, baraza hilo la wawakilishi la Marekani lilipiga marufuku
ununuzi wa maji mazito kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Miswada hiyo
dhidi ya Iran ya Kiislamu imepitishwa katika hali ambayo Rais Barack
Obama wa Marekani ametishia kuipigia kura ya veto kuipinga.
0 comments:
Post a Comment