Nyoka Mkubwa Aliyekamatwa katika eneo la ujenzi huko nchini Malaysia inasemakana kuwa mrefu zaidi ya wote waliowahi kukamatwa Duniani, Takwimu zinazoonesha urefu wa mita 8 alizokuwa nazo nyoka huyo zinatosha kabisa kumfanya mrefu zaidi katika viumbe jamii ya reptilia. Nyoka huyo alikamatwa katika mji wa Paya Terubong sehem ilipokuwa ikijengwa barabara ya juu "flyover"
Kifo cha nyoka huyo kinamuingiza katika rekodi za ushindani wa nyoka mrefu zaidi duniani
Msemaji wa serikali ya Malaysia anasema wafanyakazi katika ujenzi wa barabara waliomba msaada kupitia simu juu ya uwepo wa kiumbe hiko eneo la kazi na iliwachukua dakika 30 kumkamata nyoka huyo
"Nyoka huyu ana urefu wa mita 8 na uzito wa kilo 250" Alisema
Kitabu cha kurekodi matukio "The Guinness Book of World Records" kinamuandika nyoka huyu kuwa mrefu zaidi duniani akimpiku nyoka aina ya Medusa aishie Makumbusho ya Kansas mwenye urefu wa mita 7.67 na uzito wa kilo 158.8 pungufu ya kilo 90 za nyoka huyu (hii rekodi ilichukuliwa mwaka 2011) Kuanzia mwaka 2016 nyoka huyu ndo anashika rekodi mpya ya dunia
0 comments:
Post a Comment