pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Yai La Pili kwa Ukubwa Kuliko Mayai Yote Duniani

KUKU anayefahamika kwa jina la Matilda ambaye ametaga jumla ya Mayai 4 tu ametokea kutaga yai Kubwa mno linalokisiwa kuwa mara 4 ya yai la kawaida.
Mmiliki wa KUKU huyo Mark Cornish, anasimulia ya kwamba yai hilo lina urefu wa sentimita 9( Inchi 3.5) na lina upana wa sentimita 21(Inchi 8.3).
Bwana  Cornish, mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Ipswich, anadai kushtushwa na ukubwa wa yai hilo alipolikuta shambani kwake
''Nilishtuka sana, nilihisi mnyama mweupe kalala kwenye kiota cha kuku kwa bahati mbaya ,'' Alisema.
''Yai halikuonekana kutagwa na kuku yule. Nahisi ni kubwa mara 4 ya yai la kawaida"

''Tatizo hili yai ganda lake ni jepesi mno. Tayari linaonekana kuwa na ufa kwahiyo inabidi nilile usiku huu.

Msemaji wa kitabu cha rekodi  "Guinness World Records" alisema '' yai kubwa duniani lilikuwa na urefu wa sentimita 31   (Inchi12.2) na upana wa sentimita  22.8 (Inchi 9) huku likiwa na uzito wa gramu  340(12oz).

''Yai hili lilitagwa na KUKU aliyefahamika kama  Black Minorca katika shamba la Bwana   Stafford Damsteads huko Mellor Lancs Mwaka 1896.''

0 comments:

Post a Comment