UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.
Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.
Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mah a k a - mani kutoa ushahidi wa kile a l i - chokisema.
“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.
Katika mahoj i a n o na kituo kimoja cha redio hivi karibuni Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.
“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.
Manara alisema anashangazwa na mchezaji huyo badala ya kucheza mpira anazungumza taarab.
Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.
Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.
Awali, Kamati hiyo ilisikiliza kesi hiyo na kumtaka Kessy kuilipa Simba dola za Marekani 60, 000 lakini Simba walisema wanahitaji walipwe dola 600,000 kama fidia ya kuvunja mkataba ikiwa ni kipengele ambacho kipo kwe - n y e m k a t a b a kati yao kwa atakayevunja mkataba at amlipa mwenziwe fedha hizo.
Simba inadai kuwa mchezaji huyo alisaini Yanga Juni 15 na kwamba ina vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na mchezaji huyo kuvaa jezi za Yanga na kusafiri na timu hiyo Uturuki kabla ya Juni 20 ambayo Yanga inadai ndio siku iliyomsajili mchezaji huyo.
Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.
0 comments:
Post a Comment