Kibaka Anaswa
Kijana
anayejulikana kwa jina moja la Emmanuel (30), amejikuta akipokea
kipigo kizito baada ya kukamatwa akiiba katika Chuo cha Theofilo
Kisanji ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar.
Tukio
hilo lilitokea hivi karibuni kanisani hapo, mchana kweupe ambapo Kibaka
huyo ambaye amekuwa akifika mahali hapo mara kwa mara, alijikuta
arobaini yake ikitimia na hivyo kutiwa mikononi mwa wanachuo ambao kabla
ya kuhoji zaidi, walimshushia kipigo cha mbwa mwizi.
“Huyu
ndiye huwa anatuibia humu chuoni na kanisani, kila siku watu
wanalalamika kuibiwa vitu vyao. Juzi tu, kuna watu waliibiwa simu,
wengine fedha lakini hatukujua ni nani aliyekuwa akitufanyia hivyo, sasa
huyu tutamkomesha,” alisema dada mmoja huku akiwa na furaha ya
kukamatwa kwa jamaa huyo.
Wanachuo
hao, wakionekana kupania kumfundisha adabu na kumwachisha Emmanuel
udokozi, walikuwa wakimhoji maswali Kibaka huyo huku wakimwangushia
kipigo mfululizo, hali iliyosababisha mwili kutoka damu nyingi
iliyotapaa sakafuni kama buchani.
Kama
kawaida, vijana wetu hawakutaka kuishia kuangalia kipigo tu, waliwaita
baadhi ya wanachuo walioibiwa mali zao na mashuhuda waliomuona kibaka
huyo akiiba na kueleza mchezo mzima ulivyokuwa.
“Nilikuja hapa chuoni saa tisa (alasiri) nikaelekea mapokezi na baadaye darasani.
Nilipofika
hapo, nikamuona mtu akisimama ghafla, nikashtuka lakini sikutaka kuwa
na wasiwasi sana, nilidhani ni mwanachuo wa hapa,” alisema msichana
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Adolphina na kuendelea:
“Nikaondoka
hapo na kupanda juu (ghorofani). Moyo wangu ukawa mzito, ghafla
nikajikuta nikishuka ngazi na kurudi kule mapokezi. Nilipofika mapokezi,
yule mtu niliyemuona pale hakuwepo, nilipoanza kumtafuta, nikaona
akielekea getini kwa mwendo wa harakaharaka, hapo ndipo nilipoanza
kupiga kelele za mwizi, naye akaanza kukimbia mpaka alipokamatwa,”
alisema Adolphina.
Kibaka
huyo alipopekuliwa begi alilokuwa nalo alikutwa na vyeti mbalimbali vya
shule ya sekondari ya mkoani Mbeya, cheti cha kuzaliwa, cheti cha TRA
na vyeti vingine vingi, vyote vikiwa si vyake.
Mbali
na vyeti hivyo, pia alikuwa na kadi za mashine za ATM zikiwepo za CRDB,
NMB na NBC, hali iliyoonesha kwamba huwa anazitumia kwa ajili ya
kuchukulia ‘mkwanja’ kutoka katika akaunti za watu.
Alipopekuliwa
zaidi mifukoni mwake alikutwa na simu aina ya Huawei yenye thamani ya
shilingi 360,000 na Nokia Asha yenye thamani ya shilingi 150,000, ambazo
zote ziliibwa ndani ya chuo hicho siku chache zilizopita.
Askari
wa Kituo cha Polisi Kijitonyama – Mabatini ndiyo walimuokoa jamaa huyo
mikononi mwa wanachuo hao ambapo walifika eneo la tukio baada ya
kujulishwa na mmoja wa watu walioshuhudia jamaa huyo akisulubiwa kwa
hasira.
BY,GUMZO
0 comments:
Post a Comment