Diwani wa Isakamaliwa, Igunga, Doto Kwilasa, Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Erasto Shokoro, wajumbe sita wa serikali ya kijiji na mtu ambaye hajajulikana wamenusurika kuchomwa moto na wananchi.
Wananchi hao waliwafungia ndani ya chumba cha mikutano
viongozi hao kwa madai ya kuitisha kikao cha kuwazuia vijana wa
Isakamaliwa wasilipize kisasi kwa wafugaji waliowachoma mikuki vijana
wenzao.
Vurugu za kutaka kuchoma moto
chumba hicho zilitokea juzi katika Kijiji cha Isakamaliwa baada ya
makundi mawili ya wafugaji wa kata hiyo kutofautiana na kusababisha
kundi moja kushambulia jingine kwa mikuki wakidaiwa kuingiza mifugo
kinyume cha sheria katika bonde la Magogo.
Credit, tanzania daima
0 comments:
Post a Comment