Na Heri Shaaban
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake wote kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa
uhakiki ili kubaini kama kuna vyeti feki.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Job Masima, aliyasema hayo Dar es
Salaam jana wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Hifadhi ya
Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA).
Alisema kuanzia leo,
watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa kuwasilisha vyeti vya
vyuo walivyosomea."Natoa mwezi mmoja kuanzia leo hadi Januari, wawasilishe
yeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada ya ukaguzi tutafuatilia maeneo
waliyosomea ili kubaini kama kuna
askari wanaotumia vyeti
feki," alisema.
Alisema askari ambao
watabainika kutumia vyeti feki na kupata vyeo wakiwa kazini, watashushwa vyeo
ambapo lengo a ukaguzi huo ni kuwataka watumishi hao kusomea katika vyuo
vinavyotambulika na Serikali si vya mitaani.
Aliongeza kuwa, mpango huo
pia utawahusisha watumishi ambao wamesomeshwa na Wizara ambao nao watatakiwa kwasilisha
vyeti vyao upya.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka,
aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa
ajili ya kuweka mafao yao.
Alisema kuna mifuko mingi
hivyo kila mtumishi anaweza kuchagua wowote anaopenda kujiunga nao ili uweze kumsaidia
dhidi ya matukio yasiotarajiwa.Matukio hayo ni pamoja na maradhi, ulemavu,
kustaafu kazi,kuacha kwa hiari au kwa lazima. Akizungumzia changamoto zilizopo
katika sekta hiyo, alisema takwimu zinaonyesha wananchi walio katika sekta
rasmi wanakadiriwa kufikia
milioni 1.5 ndio wananufaika
na sekta hiyo.
MAJIRA
0 comments:
Post a Comment