Picha zilizonaswa na mtambo wa satelite wa Thailand
Mtambo wa Satelite nchini
Thailand umenasa picha za mabaki 300 yanayodhaniwa kuwa ya ndege ya
Malaysia MH370 iliyopotea wiki tatu zilizopita.
Picha hizo zilinaswa tarehe 24 mwezi Machi, Siku
moja baada ya mtambo wa Satelite wa Ufaransa kunasa picha zengine za
mabaki 122 yaliyodhaniwa kuwa ya ndege hiyo.Ndege MH370, ilitoweka tarehe 8 mwezi Machi, ikiwa na watu 239.
Wataalamu nchini Australia wanaendelea na juhudi za kuitafuta ndege ya Malaysia
Hakuna taarifa rasmi za mabaki hayo kuonekana baharini.
Msako ulifanywa kwa kutumia ndege na meli ingawa shughuli hiyo ilisotishwa nchinio Australia, Alhamisi kutokana na hali mbaya ya hewa.
Hata hivyo meli nchini Australia zinaendelea na shughuli hiyo licha ya hali kuwa mbaya.
Duru zinasema kuwa picha hizo zimekabidhiwa kwa serikali ya Malaysia hasa maafisa waliokuwa wanaendesha shughuli ya kuitafuta ndege hiyo.
Hata hivyo vifaa hivyo havijathibitishwa ikiwa ni mabaki ya ndege ya Malaysia iliyotoweka
bbc
0 comments:
Post a Comment