Wanamgambo walioteka bandari ya
nchini Libya wameiambia BBC kuwa wameanza kusafirisha mafuta kwenda nchi
za nje kwa meli ya kwanza iliyopeperusha bendera ya Korea ya Kaskazini.
Naibu wa Waziri wa Mafuta ameithibitishia BBC
kuwa meli hiyo ya mafuta Morning Glory ilitia nanga katika bandari ya
Sidr iliyochini ya himaya ya wanamgambo.Uwezo wa serikali ya Libya kuhuisha biashara ya kusafirisha mafuta nje ya nchi ambayo ni muhimu kwa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo zilikumbana na vikwazo vya migomo na maandamano na bandari na visima vya mafuta kutekwa na wanamgambo maeneo mbali mbali nchini humo.
BBC
0 comments:
Post a Comment