MAHAKAMA
ya Rufaa Dar es Salaam, imetengua adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela
na faini ya sh bilioni 22 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam Februari 23 mwaka 2012, dhidi ya raia wa Taiwan na China.
Nahodha wa meli, Hsu Chin Tai, na wakala wa meli ya Tawaliq 1, Zhao
Hanquing walikata rufaa baada ya kubaini sheria zilikiukwa wakati wa
uendeshwaji wa kesi hiyo katika mahakama za chini.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na jopo la majaji watatu Salum Masati,
Semistocles Kaijage ambao walisema dosari ya kwanza ambayo Mahakama ya
Rufaa imebaini ni kwamba kesi hiyo ilifunguliwa bila kibali cha
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Hata hivyo, Mahakama Rufaa imempa ruhusa DPP ya kuwafungulia kesi
upya warufani hao na wale walioachiliwa na Mahakama Kuu, kama ataona
kuna haja ya kufanya hivyo.
Wakili wa warufani hao, John Mapinduzi, alisema amefurahishwa na
hukumu hiyo na kwamba hivi sasa anajiandaa kufungua kesi ya madai dhidi
ya serikali kutaka wateja wake walipwe fidia.
Pia alisema ataiomba Mahakama iilipe meli iliyokuwa ikitumiwa na
watuhumiwa hao kuvua samaki ambayo kwa sasa imechakaa kutokana na vyuma
vyake kukatwa kama chuma chakavu.
Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa
na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina
kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
freemedia.co.tz
0 comments:
Post a Comment