Ilisemekana
kwamba akiwa na mjumbe wa kitongoji hicho, mzazi huyo aliyepata fununu
kuwa mwanaye wa kiume analawitiwa na mzee huyo, alifanya jitihada za
kumsaka mzee huyo hadi kibaruani kwake ambapo alipohojiwa kama
amemfungia mwanafunzi wake ndani ya chumba chake, mzee huyo alijiumauma
na mwishoni kukubali.
Ilidaiwa
kwamba wananchi na mzazi wa mwanafunzi huyo walimbeba mzee huyo
msobemsobe hadi nyumbani kwake na kumtaka amfungue denti huyo ambapo
alifanya kama alivyoagizwa kisha mwanafunzi huyo alichomolewa ndani ya
chumba hicho.
Ilidaiwa
kuwa kabla hata majibu ya daktari hayajachukuliwa, Mzee Kijana
alionekana akirandaranda mitaani, jambo lililosababisha viongozi wa mtaa
huo kuwasiliana na polisi kuhoji kulikoni?
Ilielezwa kuwa wakati wakuu hao wakihangaika na suala hilo ndipo wananchi wenye hasira kutoka kila upande waliivamia ofisi hiyo wakidai kuwa wamechoshwa na rushwa za wazi zinazofanywa na viongozi wao na kudai kuwa watampa adhabu mzee huyo wao wenyewe.
Ilielezwa kuwa wakati wakuu hao wakihangaika na suala hilo ndipo wananchi wenye hasira kutoka kila upande waliivamia ofisi hiyo wakidai kuwa wamechoshwa na rushwa za wazi zinazofanywa na viongozi wao na kudai kuwa watampa adhabu mzee huyo wao wenyewe.
Ilidaiwa
kwamba kufumba na kufumbua, watu hao wasio na idadi walivunja mlango na
kumchomoa Mzee Kijana aliyekimbilia ofisini humo kwa ajili ya hifadhi
na kuanza kumshambulia kwa kila aina ya silaha kiasi cha almanusura
kumuua.
Kipigo
hicho kilisababisha askari waliofika hapo ili kutuliza ghasia, kushindwa
kazi, jambo lililowalazimu kutoka nduki ili kuokoa roho zao.
Akizungumza na wanahabari wetu, mwenyekiti wa mtaa huo, Mohamed Chande
alisema kuwa ilibidi aikimbie ofisi yake kwa kuwa watu walikuwa na
ghadhabu kupita maelezo.
Inadaiwa
kuwa msamaria mwema mmoja alimnyakua Mzee Kijana kutoka katika kundi la
watu na kumpakiza kwenye gari lake haraka na kumsalimisha mikononi mwa
Polisi wa Kizuiani ambapo inadaiwa kuwa hadi sasa yupo huko.
Akizungumza
na waandishi wetu, bibi wa mwanafunzi huyo anayedaiwa kulawitiwa
aliyejitambulisha kwa jina moja la Rugwesi (38), alisema kuwa alishangaa
kuona mtuhumiwa akiachiwa kwa dhamana siku chache kabla hata majibu ya
daktari hayajatoka.
“Ripoti
imeonesha kuwa mjukuu wangu alikuwa akilawitiwa kwa muda mrefu na mzee
huyo na si mjukuu wangu tu inadaiwa anawafanyia hivyo wanafunzi wengine
watatu,” alisema bibi huyo huku simu ya mkuu wa Kituo cha Polisi
Kizuiani ikiita bila kupokelewa.
SOURCE: GPL
0 comments:
Post a Comment