Mtu mmoja Hamisi Mayala anayekadiriwa kuwa na umri kati ya
miaka 58 hadi 60 amefariki dunia baada ya kuuawa na wananchi wanaodaiwa
kuwa na hasira kali katika kijiji cha Kilago wilayani Kahama Mkoani
Shinyanga kutokana na kusadikika kuwa ameiba mahindi mabichi.
Akizungumza na Redio Kahama Diwani wa Kata ya Kilago Peter Emanuel
amesema Tukio hilo limetokea juzi Majira ya saa 12 jioni baada ya baadhi
ya wananchi kumkuta akivunja mahindi katika shamba ambalo
halijafahamika kuwa ni la Nani.
Amesema wananchi hao wakipiga kelele ndipo umati wa watu ulijaa na
kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi hadi kuumuua na kwamba wananchi
walisambaa baada ya kuona mtuhumiwa huyo amepoteza maisha.
Diwani Emmanuel amesema amepata taarifa kutoka kwa viongozi wake wa
kijiji, na kuchukua jukumu la Kupiga simu Polisi ambao wamefika jana
asubuhi na Kuuruhusu mwili wa marehemu uzikwe kwa kuwa ndugu zake
hawakufahamika mara moja.
Amesema Marehemu Mayala ameingia kijijini hapo mwaka Juzi na alikuwa
anaishi katika nyumba ya kupanga huku akijishughulisha na kufanya
vibarua kwa wakulima wa kijiji hicho na inadaiwa alitokea katika Tarafa
ya Msalala Wilayani Kahama.
Hata hivyo Diwani Emmanuel amewataka wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi na dabala yake wawafikishe watuhumiwa sehemu
inayohusika, huku akiahidi kulisaidia jeshi la polisi kutoa elimu kwa
wananchi.
Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukia
hilo na linaendelea na Uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na mauaji hayo
ya kujichukulia sheria mkononi na kuwafikisha katika mikono ya sheria.
0 comments:
Post a Comment