pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Zanzibar ndani ya Tanganyika au muungano?

ASP-TANUNianze kwa kunukuu tangazo nililokuta Bagamoyo, nilipokwenda katika shughuli zangu za kutoa ushauri kuhusu maendelezo bora ya ardhi eneo la makurunge ili kunogesha mjadala katika makala yangu leo ubaoni.

Tangazo liliandikwa hivi “TAHADHARI! USIKUBALI KUNUNUA ARDHI/SHAMBA KATIKA ENEO LILILOKUWA SHAMBA LA RAZABA. SHAMBA HILI LINALOAMBAA KATIKA MAENEO YA MAKANI, MAKURUNGE, GAMA NA MTO WAMI NI SHAMBA LA SERIKALI NA TAYARI LIKO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUMILIKISHWA KWA KAMPUNI YA UWEKEZAJI YA ECOENERGY” Mwisho wa kunukuu.
Tangazo hilo liliwekwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo tarehe 21 Novemba 2011 na kuibua hoja zangu kubwa mbili. Kwanza RAZABA ni nini na Serikali ni nani maana tangazo linasema shamba lililokuwa la RAZABA pia inataja shamba la Serikali na kwa nini matumizi yake yanabadilishwa.Pili watu wasinunue ardhi katika eneo hilo kutoka kwa nani? Kuna raia wanaishi humo? Kwa amri ya nani na waliingiaje humo?

Maaana halisi ya neno RAZABA ni Ranchi ya Zanzibar, Bagamoyo (Ranch of Zanzibar in Bagamoyo)Kwa simulizi kutoka kwa watangulizi wetu eneo la RAZABA ilikuwa ni zawadi ya Mwalimu Nyerere kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na lina ukubwa wa zaidi ya hekta elfu ishirini na nane.
Mto Wami, reli ya Tanga, Barabara ya Bagamoyo Msata, mto ruvu na bahari ya hindi ndio mipaka halisi ya RAZABA. Mmiliki wa RAZABA ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kwa maana halisi, RAZABA ni eneo la Zanzibar ndani ya Tanganyika.
Hayati Mwalimu Nyerere alitoa eneo hilo ili kuwapa fursa Wazanzibari kumiliki mifugo yao wenyewe, na mifugo yote inayotoka maeneo ya Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma na kwingineko kwenda Zanzibar, ifikie RAZABA kabla ya kusafirishwa kwenda kutumiwa na wananchi wa Zanzibar.
Leo biashara ya ardhi kati ya RAZABA na ECOENEGY inafanywa na nani? Serikali ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar? Kwa manufaa ya nani? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanganyika au Serikali ya muungano? Matumizi yaliyopangwa wakati wa kutenga eneo la RAZABA hivi sasa yamepitwa na wakati?
Wananchi wa Zanzibar hivi sasa wamesitisha ulaji wa nyama kutoka bara au wamepata mbadala? Lakini kwa kutumia akili ndogo kabisa, hivi mbadala wa nyama Zanzibar zaidi ya kuitegemea Tanganyika ni upi? Upo kweli? Kulikuwa na mantiki kubwa sana kuweka rachi katika eneo linalosemwa lilikuwa la RAZABA.
Kwanza kuna reli ambayo inarahisisha usafirishaji wa mifugo kutoka bara inapopatikana kwa wingi, kuna mito miwili inayofanya urahisi wa kupatika kwa maji kwa ajili ya mifugo, barabara ni ya uhakika lakini kikubwa zaidi, Bahari ya Hindi inayounganisha Visiwa vya Zanzibar na Mji wa Bagamoyo.
Pia kwa mtazamo wa mbali tungejenga hata kiwanda cha kusindika nyama na samaki ili tutumie vyema bandari kubwa inayojengwa Bagamoyo kuuza nyama iliyosindikwa nje ya nchi. Leo tunapoiua RAZABA, mbadala wake ni nini?
Sina maana ya kupinga mradi au uwekezaji wa kilimo cha miwa kwa ajili ya nishati mimea (bio fuel) unaokuja kufanywa na ECOENERGY, lakini kwa ardhi yote tuliyonayo Tanzania tunashindwa kuwatafutia ECOENERGY eneo jingine ambalo halijawahi kupangiwa matumizi?
Chanzo: Mwananchi

0 comments:

Post a Comment