Mahabusu wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha,
kaskazini mwa Tanzania, Jumanne walisababisha vurugu katika viwanja vya
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo baada ya kuvua nguo na kugoma
kushuka kwenye basi lililowachukua kwenda mahakamani wakipinga kitendo
cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa huru.
Watuhumiwa wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara
mbili ili wapewe dhamana ni Dharam Patel na Nivan Patel wanaodaiwa
kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili,2014.
Kwa mujibu wa watu waliokuwa katika eneo la mahakama hayo, mahabusu
hao walikuwa wakipaza sauti kupinga madaraja(ubaguzi) miongoni mwa
watuhumiwa, wenye uwezo kifedha na wasio nacho, hali ambayo imesababisha
wengine kuachiwa na wengine kuendelea kusota magerezani kwa kisingizio
cha “upelelezi haujakamilika”
Mahabusu hao walisikika wakipaza sauti kutoka ndani ya basi: “Wenzetu
hata mwezi haujaisha wanafutiwa kesi, jamani sisi tumekosa nini?
Tunataka haki itendeke kwa wote” walisema.
Kuachiwa kwa watuhumiwa wanaolalamikiwa na mahabusu wenzao
kunasemekana kumetokana na hatua ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka
Arusha kubadilisha hati ya mashitaka na hivyo kuwawezesha kupata
dhamana.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey
Nzowa ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa ofisi yake haina taarifa za
watuhumiwa hao kupewa dhamana lakini alisema kulikuwa na jaribio la
kufanya hivyo.
Bwana Nzowa amesema baada ya kubainika njama hizo, ofisi yake
ilipinga, akisema kuwa kosa la watuhumiwa lilikuwa wazi na hivyo
kuonyesha hali ya kutoamini kuwa watuhumiwa wanaweza kupata dhamana kwa
kosa hilo!
Hata hivyo Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, DPP haijaweza kulitolea
maelezo suala la mahabusu hao kulalamikia mahabusu wenzao kupendelewa
katika utoaji wa haki kwa makosa wanayotuhumiwa.
SHAME SHAME POLICE N MAJISTRATE...THERE HAS TO SAME JUSTICE RATHER INFLUENCED/PURCHASED VIA MONETARY GAINS...
ReplyDelete