Hai. Kijana aliyetambulika kwa jina la Yusufu Njau (32) mkazi wa kijiji cha Roo Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, ameuawa kwa kuwakatakata mapanga wazazi wake na kisha kuchoma nyumba moto na kukimbia kusikojulikana.
Mauaji hayo yaliyotokea juzi saa 12:30 jioni
yamesababisha simanzi kubwa katika kijiji hicho na kuwalazimu wananchi
wa kijiji hicho kuanza kumsaka kijana huyo usiku kucha bila mafanikio.
Mwenyekiti wa kijiji cha Roo, Alfani Swai
amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo alisema mpaka sasa chanzo
cha mauji hayo hakijafahamika na kuwataja waliopoteza maisha kuwa ni
Shahidu Njau (60) na mkewe Minae Swai (57) .
Swai alisema wananchi waliamini nyumba imewaka moto kwa bahati mbaya lakini ghafla waliona mwili wa mwanamke ukiwa chini umetapakaa damu na umekatwakatwa kila mahali.
Alisema waliusogelea na kuugusa na kubaini tayari
amefariki dunia na walipoangalia mbele waliona mwili wa mwanamume ukiwa
umepasuliwa kichwa na ubongo uko nje huku akihema kwa shida ambapo
walijitahidi kumwahisha hospitali na alipofika eneo la Sadala alipoteza
maisha.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Norvatus Makunga ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo alisema mpaka
sasa sababu za kijana huyo kufanya mauaji makubwa kiasi hicho
hazijajulikana .
Kamanda wa polisi mkoani hapa Robert Boaz
amethibitisha kutokea kwa mauji hayo na kusema Jeshi la Polisi
linaendelea kumsaka kijana huyo ili hatua za kisheria ziweze
kuchukuliwa.
0 comments:
Post a Comment