Polisi nchini Marekani wamethibitisha kuwa kijana Elliot Rodger
mwenye miaka 22 ambaye ni mtoto wa mtengeneza filamu maarufu, ndie
aliyefanya mauaji ya watu sita kwa pamoja jijini Califonia.
Kijana huyo ambaye ni mwanafunzi ni mtoto wa Peter Rodger ambaye ni
mtayarishaji filamu wa Marekani aliyesaidia kutengeneza filamu ya The
Hunger Games.
Polisi wamesema kuwa kijana huyo aliwachoma visu wanafunzi watatu
aliokuwa akishare nao chumba kwenye nyumba yake ambapo baadae alikwenda
katika duka moja na kuanza kurusha risasi mfululizo zilizojeruhi watu na
kusababisha vifo.
Baada ya tukio la kurushiana risasi na polisi Rodger alikutwa amekufa
ndani ya gari lake lililopata ajali akiwa na majeraha kadhaa ya risasi
kichwani.
0 comments:
Post a Comment