Geita.
Zaidi ya nyumba 24 zimevunjwa na
kuteketezwa moto Kijiji cha Kilombero, mkoani Geita na wananchi kutokana
na mauaji ya Felister Mathias (55), anayedaiwa kuuawa kwa kukatwa
mapanga na watu wa ukoo mmoja.
Taarifa zinadai ukoo huo umekuwa tishio kijijini
hapo, kwani zaidi ya watu watano wameuawa kwa miezi mitatu kwa kukatwa
panga na ukoo huo.
Kutokana na tuhuma hizo, wananchi hao waliingiwa
na hasira na kuamua kuchoma nyumba nne za ukoo huo na zingine 20 za
wananchi ambao walishindwa kujiunga nao baada ya kupigwa yowe kutokana
na kuuawa kwa Mathias.
Akisimlia tukio hilo, mtoto wa marehemu, Christina
Charles alisema kabla ya kuuawa kwa mama yake kulikuwa na ugomvi kati
yake na mmoja wa wanaukoo hao, ambaye pia ni Katibu wa Sungusungu kwa
kile kilichodaiwa ng’ombe wao waliingia kwenye shamba lake. “Kabla mama
hajauawa tulikuwa na ugomvi ambao ulitokana na kijana wetu kulisha
ng’ombe kwenye shamba la... hali hiyo ilisababisha kuwapo mgogoro ambao
tulilipa fidia ya Sh40,000,” alisema Charles.
Charles alisema licha ya kulipa faini, mwanaukoo
huyo aliendelea kuwasumbua na kuamua kuhamishia ng’ombe wao eneo la
Katoro. Mwenyekiti wa kijiji hicho, Sospeter Bulengeti alikiri ukoo huo
ni tishio kwani ni wakorofi na kwamba, ni wahamiaji kutoka Kijiji cha
Msalala, Wilaya ya Nyang’hwale.
“Tuliamua kupiga kura zaidi ya watu 300
walishiriki, 20 walipigiwa kura huku ukoo huo ulipata kura nyingi zaidi
ya 70,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita,
Manzie Mangochie alipiga kambi eneo hilo huku akitoa siku 10 wahusika
kukamatwa.
Hata hivyo, amri hiyo imesababisha wanaume
kukimbia kwa hofu ya kukamatwa kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ilipokwenda kijijini hapo, ilikuta
wanawake wachache na watoto, hali iliyosababisha kushindwa kufanya
mkutano wa hadhara.
peke yao ambapo wakati kamati ya ulinzi wilaya
inaenda kijijini hapo ilishuhudia kikiwa na wanawake wachache na watoto
jambo lililowapa wakati mgumiu wakufanya mkutano wa hadhara na kuamua
kuacha.
Pia inaelezwa kwamba tatizo la wananchi
kujichukulia sheria mkononi ni uelewa mdogo wa sheria na huku wengine
wakidai kuwa jeshi la polis haliwachukulii hatua wanaohusika na uvunjaji
wa sheria na pia umbali wa vituo vya polisi jambo linalosababisha
kuamua kuwadhibiti waharifu kwa kujichukulia sheria mkononi.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment