ng'ombe akikimbia katika korido za hospitali |
Ktika hali isiyo ya kwaida Ng'ombe mmoja ameingia hospitalini nchini Brazil na kuzua taharuki kubwa kwa manesi na wagonjwa hospitalini hapo,
Manesi na wagonjwa walianza kukimbia hovyo kwenye korido za hospitali hiyo wakihofia maisha yao,
mkanda wa video kupitia kamera za CCTV zimeonesha wagonjwa waliokuwa wakiumwa sana nao wakijitahidi kukimbia kuokoa maisha yao
tukio hilo limetokea katika hospitali ya Francisco Limongi iliyopo Rio de Janeiro.
Katika video hiyo pia walinzi waliokuwa zamu wameonekana wakicheka wakati ng'ombe huyo akiingia hospitalini hapo kwa kasi ya ajabu mno, pia video hiyo imemuonesha kiumbe huyo akivunja milango ya hospitalini hapo na kuwakimbiza manesi kama watatu ambao walionekana kuogopa sana tukio hilo
bahati nzuri hakiuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo na baadae ng'ombe huyo alikamatwa na kurejeshwa katika zizi lake karibu na hospitali hiyo
SOUTH AFRICA
Katika tukio lingine la aina hiyo twiga mwenye urefu wa futi 20 alitoroka katika hifadhi huko afrika ya kusini na kuingia katika mgahawa uliokuwa jirani,
tukio hilo lilitokea mapema mwezi wa pili mwaka huu, watalii wengi walisema hawajawahi kuona tukio kama hilo katika maish ayao ya kitalii, walishangazwa jinsi twiga huyo alivyoweza kujipinda na kuingia mahali pale
0 comments:
Post a Comment