KANISA Katoliki duniani limeamua kufunga zaidi ya parokia 50 katika Jimbo Kuu la KanisanKatoliki la New York nchini Marekani, katika mkakati wa kanisa hilo kujinusuru na madeni ya
parokia zisizojiendesha, ambao haujawahi kufanyika katika miaka 164 ya jimbo hilo. Miongoni mwa parokia zitakazofungwa ni ile ya East Harlem, ambayo ndiyo kanisa la kwanza kukaribisha waumini kutoka Puerto Rico Parokia nyingine ni ya Upper East Side, iliyoanzishwa kwa sadaka ya Dola za Marekani 50 kutoka kwa waumini na wafanyakazi kutoka Italia katika miaka ya 1920. Pia lipo kanisa pekee linaloendesha misa kwa lugha ya Kilatini kila siku, lenye umri wa miaka 150 lililopo Midtown.
Aidha, inatarajiwa mwaka ujao zaidi ya parokia zingine 50, zitafanyiwa marekebisho makubwa, ikiwa ni pamoja na kuunganishwa na parokia
zingine. Mpango huo wa kufunga makanisa ni sehemu ya mchakato wa kubadili sura na mwelekeo wa Kanisa la New York kiutendaji, ulioanza mwaka
2010. Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, makanisa yatakayofungwa yatatamkwa leo katika misa Jumapili kwenye makanisa yote ya Jimbo hilo.
Tayari vuguvugu la upinzani dhidi ya hatua hiyo, limeanza hasa kwa makanisa yaliyo katika hatari ya kufungwa, kutokana na kutofikia vigezo
vilivyowekwa na utawala. Jimbo Kuu hilo, lina parokia 368 katika maeneo ya Bronx, Manhattan, Kisiwa cha Staten na kwenye kaunti saba zilizopo Kaskazini mwa Jiji.vMwaka 2007 Kadinali Edward Egan alifunga parokia 21 na kusababisha kuibuka kwa upinzani mkubwa miongoni mwa waumini, ambao bado unaendelea katika baadhi ya parokia. “Baadhi ya waumini wetu watahuzunika watachanganyikiwa na hata kukasirika,” alisema mrithi wa Kadinali Egan, Askofu Mkuu, Kadinali Timothy Dolan na kunukuliwa na gazeti la Wakatoliki la New York kuhusu mabadiliko hayo.
Alisema anaelewa ugumu wa hali hiyo, kwani waumini wengi wanatambua kwamba parokia hizo ndio mama wa imani na Wakatoliki wanazithamini hivyo uamuzi huo utawauma. Sababu za kufunga parokia hizo, zimetajwa
kuwa ni zile zile za mwaka 2007, ikiwamo yavkupungua kwa idadi ya mapadri wa kuhudumia katika parokia, tatizo la kifedha, kupungua kwa idadi ya Wakatoliki wanaobatizwa, kuoa au
kuolewa kanisani. Dayosisi ya Brooklyn ambayo hujumuisha makanisa ya Queens, ilikabiliwa na tatizo hilo na kuchukua hatua za kufunga baadhi ya parokia zake kutoka 199 hadi 187 kwa mwaka 2009. “Hatuna fedha kila mwaka tunatoa dola milioni 40 kusaidia parokia zisizohitajika,” alisema Kadinali Dolan katika blogu yake mwaka jana.
Kwa mujibu wa habari za ndani, paroko ambao parokia zao zitafungwa wameshaambiwa hatua hiyo tangu juzi na leo katika makanisa yote, kutakuwa na taarifa kwa Wakatoliki.bMwaka jana paroko hao walitembelewa na kutakiwa wakusanye waumini wao, ili kuthibitisha uwezo wao au udhaifu wao ambapo baadhi walishauriwa kujadiliana na parokia jirani kuhusu walichokiona.bBaadaye kamati za ushauri zilizojumuisha mapadri na waumini wa kawaida, zilipitia taarifa
hizo na kuzitolea mapendekezo Aprili mwaka huu ambayo Juni mwaka huu yalifikishwa kwa Kadinali.
Akizungumzia hali hiyo kwa hapa nchini, KatibuvMtendaji wa Idara ya Mawasiliano Jamii wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Anatoly
Salawa alisema kwa Tanzania kwa sasa hakuna Parokia inayoshindwa kujiendesha, kutokana na tatizo la fedha. Hata hivyo, alikiri baadhi ya Parokia ambazo si za mjini, zipo zisizo na fedha nyingi kama mjini,nlakini zinajiendesha kwa uwezo wake “Parokia ikishindwa kujiendesha ni sawa na waumini wameshindwa kuendesha familia zao, kwani wao ndio Parokia na wanapaswa kuhakikisha inafanya kazi”, alisema.Akitetea hoja ya Parokia za nchini ni vigumu kushindwa kujiendesha, Salawa alisema hali hiyo
inatokana na kuanzishwa kwa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki na Kati (AMECEA).
Anasema Shirikisho hilo lilianzisha jumuiyabndogondogo mwaka 1976, ambazo zimelenga waumini kufahamiana na kusaidiana. Alisema hali hiyo inasaidia kuokoa Parokia kwani ni wajibu wa waumini kuendesha kanisa. Kwa Marekani hakuna mfumo wa jumuiyanndogondogo.bKuhusu kupungua kwa idadi ya mapadri katika
Parokia za New York hivyo kuchangia kufungwa kwa Parokia hizo zaidi ya 50, Salawa alisema “hapa kwetu haijatokea hiyo na hata mapadri wetu wanaofanya kazi Marekani na Ulaya,
wameliona hilo la kupungua kwa nchi za huko”. Wiki mbili zilizopita, Kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki alionya kuwa atazifuta parokia ambazo zitashindwa kujiendesha na zinazoendeleza mitafaruku. Alisema hayo wakati wa Siku ya Dada Wadogo (watawa wa kike) wa kanisa hilo katika kituo cha dada hao kilichopo Mbagala jijini Dar es
Salaam. Alisema parokia zisizotekeleza majukumu, yanayotolewa na Mkuu wa Kanisa Katoliki, atazifuta kwa sababu zitakuwa hazina faida.
Alisema moja ya majukumu ya kila parokia ni kutoa sadaka na misaada ya kila aina kwa Dada Wadogo, hivyo parokia ambayo haipeleki kitu chochote kwao itachukuliwa hatua. “Kila parokia inatakiwa iwe imechangia ili kuwawezesha Dada Wadogo kujiendesha. Dada wadogo wanategemea Parokia kama wazazi”,
alisema
0 comments:
Post a Comment