Na
Saidi Mkabakuli
Serikali
imeweka wazi mkakati wa kuainisha fursa za kipaumbele zitakazoiwezesha kuivusha
nchi kikanda na kimataifa kwa kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya
maendeleo kama inavyobainishwa na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Miaka
Mitano (FYDP I) unaosimamiwa na Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango.
Mkakati
huo umewekwa wazi na Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi Bw.
Paul Sangawe mara baada ya kula kiapo cha kuitumika nafasi hiyo.
Bw. Sangawe amesema
kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma pamoja
na kufaidika na misaada kutoka nchi marafiki na mashirika ya kimataifa.
“Kwa mujibu wa Mpango
Wa Maendeleo Wa Taifa Mwaka 2012/13 thamani ya mauzo ya
bidhaa na huduma nje ilikuwa dola za Kimarekani 6,796.3 milioni mwaka 2011,
ikilinganishwa na dola 5,805.0 milioni mwaka 2010 sawa na ongezeko la asilimia
17.1. hivyo mkakati wetu ni kuongeza hali hii,” alisema Bw. Sangawe.
Kwa mujibu wa Mpango huo thamani ya bidhaa za kukuza
mitaji zilizoagizwa toka nje iliongezeka hadi dola za Kimarekani 3,560.5
milioni kutoka dola 2,715.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia
31.1. Ongezeko hili lilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uagizaji wa mitambo
hasa ile ya viwandani.
Aidha, thamani ya uagizaji wa
bidhaa za kati iliongezeka hadi dola za Kimarekani 4,139.0 milioni mwaka 2011,
kutoka dola 2,741.2 milioni mwaka 2010, sawa na ongezeko la asilimia 51.0.
Uagizaji wa mafuta kwa wingi ulitokana na matatizo yaliyojitokeza ya
kutozalishwa kwa kiasi kinachohitajika cha umeme unaotokana na maji, hivyo
kupelekea mitambo mingi ya mashine kuendeshwa kwa kutumia umeme unaozalishwa na
mafuta.
Vilevile, thamani ya mafuta
yaliyoagizwa katika mwaka 2011 ilikuwa dola milioni 3,228.7 ikilinganishwa na
dola milioni 2,024.2 mwaka 2010. Uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida
uliongezeka hadi dola 2,128.0 milioni kutoka dola 1,709.2 milioni mwaka 2010,
sawa na ongezeko la asilimia 24.5.
Bw.
Sangawe ameongeza kuwa Serikali inajikita katika kutambua masoko kwa bidhaa za
Tanzania na vyanzo vipya vya uwekezaji katika uchumi wa Dunia na Kikanda ili kuwezesha
sekta binafsi kuchangia kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ili
kuwezesha nchi kuchanmkia fursa za masoko ya kimataifa ikiwemo AGOA na nchi za
jumuiya za Ulaya.
“Kipaumbele
itakuwa ni kutumia rasilimali chache kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi
pamoja na kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia
uwekezaji katika maeneo ya kipaumbele na ya matokeo makubwa,” aliongeza Bw.
Sangawe.
Serikali imeaandaa Mpango wa
Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa
kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati
ifikapo 2025.
Naibu
Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) akila kiapo cha utii na
utumishi mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto).
Naibu
Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe akisaini hati ya kiapo.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete (Kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mtendaji
(Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya kumuapisha.
Watumishi
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.
Jakaya Kikwete (Watatu kushoto) mara baada ya kumuapisha Naibu Katibu Mtendaji
(Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Wapili kulia).
Watumishi
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu
Mtendaji (Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi) mpya wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Wapili kulia) mara baada ya kuapishwa.
Naibu
Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia)
akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa na kukabidhiwa jukumu la
kusimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi.
Shangwe na
vigelegele!
Watumishi
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimpokea kwa shangwe na vigelegele Bw. Paul
Sangawe (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa jukumu la Naibu Katibu Mtendaji
katika Ofisi hiyo ambaye atasimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na
Mahusianao ya Kiuchumi.
Baadhi
ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakisubiri kuapishwa
kwa Naibu Katibu Mtendaji mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul
Sangawe (hayupo pichani).
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete (Aliyeinama) akiwapa zawadi watoto wa Naibu Katibu Mtendaji
mpya wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Sangawe (Kulia) mara baada ya
kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
atakayesimamia masuala ya Biashara za Kimataifa na Mahusianao ya Kiuchumi.
Picha
zote na Saidi Mkabakuli
Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango
0 comments:
Post a Comment