Umekua ni usafiri mwingine mzuri na wenye starehe yake kama ukipata
nafasi ya kuutumia kwenye nchi zilizoendelea kama Marekani, Uingereza
Dubai na kwengineko ambako kuna watu wengine wanategemea sana kuutumia
na kuacha magari yao nyumbani na kujikuta wamewahi town na kumaliza
shughuli zao manake hamna foleni.
Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa Afrika
likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya
shilingi BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam.
Waziri
wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema
‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari
wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara
za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni
kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na
historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake?
manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.
Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na
vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake
umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Kazi
hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es
salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa
tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha
Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi
ya watu elfu moja
CRD: MILLARDAYO .COM
0 comments:
Post a Comment