pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Wamarekani katika jeshi la Israel wauawa Ghaza

Wamarekani katika jeshi la Israel wauawa Ghaza
Raia wawili wa Marekani ambao walikuwa wakipigana upande wa jeshi la Israel wameuawa katika mashambulizi ya nchi kavu ya utawala huo katika Ukanda wa Ghaza. Stuart Steinberg ambaye familia yake inaishi California nchini Marekani amesema kuwa, mwanaye aliyekuwa na umri wa miaka 24 kwa jina lal Max Steinberg ni miongoni mwa wanajeshi 13 wa Israel waliouawa huko Ghaza jana Jumapili. Jeshi la utawala wa Kizayuni pia limethibitisha kuwa wapiganaji wa Kipalestina wamemuua raia mwingine wa Marekani kwa jina la Nissim Sean Carmeli kutoka Texas aliyekuwa na cheo cha Sajenti, katika mashambulio ya Israel huko Ghaza.
Jen Psaki msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Marekani amethibitisha kuuliwa raia hao wawili wa nchi hiyo kupitia taarifa. Bridegi za Izzuddin Qassan tawi la kijeshi la harakati ya Mapambano ya Palestina Hamas hata hivyo imesema kuwa wanamuqawama wa Palestina wamewauwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wasiopungua 32 tangu Jumamosi wiki hii.

0 comments:

Post a Comment