Rais
Obama amekiri katika televishen ya kitaifa kuwa Mashirika ya Marekani
yalikosea katika kukadiria hatari ya wapiganaji wa dola ya kiislam,
Islamic State nchini Iraq na Syria.
Amesema kuwa wapiganaji hao
wenye uhusiano na Al Qaeda walitumia fursa ya kutokuwepo serikali
thabiti nchini Syria na kuongezewa nguvu zaidi na vijana waliojiunga
kupigania jihadi kutoka mataifa mengine.
Hata hivyo Obama amesema
wapiganaji hao waliwahi kuvurumishwa huko Iraq na majeshi ya nchi yake
yakishirikiana na kabila la Sunni.
Obama amekiri vyombo vya
Ujasusi vya Marekani zilikadiria vibaya uwezo wa majeshi ya Iraq
kupambana na wapiganaji wa kiislamu ambao wameteka maeneo mengi nchini
humo
0 comments:
Post a Comment