pagead2.googlesyndication.com pagead2.googlesyndication.com

Bunge kuanza wiki ijayo

MKUTANO wa 16 na 17 wa Bunge
unatarajiwa kuanza wiki ijayo, ambapo
pamoja na mambo mbalimbali, utajadili
miswada miwili binafsi, ukiwamo muswada binafsi wa mbunge maazimio matatu na Muswada wa Kamati ya Bajeti. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja alisema muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ni Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana. “Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mbunge na kamati kuwasilisha miswada na kwa upande wa Kamati ya Bajeti yenyewe itawasilisha Muswada wa Sheria ya Bajeti,” alisema Minja. Alisema pamoja na miswada hiyo pia Bunge hilo litajadili na kusoma kwa mara ya pili miswada ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) 2014, Muswada wa Sheria ya Takwimu 2013, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi 2014, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya sekta binafsi na umma 2014. Aidha, alisema mkutano huo unaotarajiwa kuanza Novemba 4 hadi Novemba 28, utajadili maazimio matatu ambayo ni azimio la kuridhia itifaki ya Afrika Mashariki kuhusu ushirikiano katika masuala ya ulinzi.nMaazimio mingine ni azimio la kuridhia itifakinya makubaliano ya msingi ya Ushirikianonkatika Bonde la Mto Nile na azimio la kuridhia Itifaki ya Uzuiaji wa Vitendo Haramundhidi yanUsalama wa Miundombinu ya kudumu iliyojengwa chini ya Bahari katika mwambao wa Bara ya mwaka 1988.Alisema Bunge hilo pia litapokea taarifa ya Kamati Teule iliyoundwa tarehe Novemba Mosi, mwaka jana, ili kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo, maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi. Akizungumzia mkutano huo, Minja alisema utakuwa ni wa wiki nne baada ya kuunganishwa kwa mikutano miwili wa 16 na 17, ambayo haikufanyika kutokana na ratiba ya mikutano ya Bunge Maalumu la Katiba. “Kutokana na mkutano huu, sasa Bunge hili limebakisha mikutano mitatu ambayo itakamilisha idadi ya mikutano 20 inayotakiwa kufanyika katika kila kipindi cha miaka mitano ya Bunge,” alisema.

0 comments:

Post a Comment