Matokeo ya kwanza kutoka kwa uchaguzi mkuu nchini Msumbiji umempa
mgombea wa chama tawala cha FRELIMO ushindi wa duru ya kwanza.
Filipe Nyusi amepata asilimia 57 ya kura hizo huku mshindani wake wa chama cha RENAMO Alfonso Dhlakama akipata asilimia 36.Renamo ambacho kinadai kulifanyika wizi wa kura kilishinda viti vingi vya ubunge kuliko awali.
Matokeo hayo yataidhinishwa na mahakama ya kikatiba kabla ya kutolewa rasmi.
Renamo na Frelimo walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu vilivyomalizika mwama 1992.
0 comments:
Post a Comment