Mbunge wa Bunge la Palestina amesema kuwa, Mwendesha Mashtaka wa
utawala wa Kizayuni wa Israel anapanga njama za kutaka itolewe hukumu ya
kifungo cha miezi 38 dhidi ya Spika wa Bunge la Palestina. Khalil
Rabi'i ambaye hivi karibuni aliachiliwa huru kutoka jela za Israel
amesema kuwa, Mwendesha Mashtaka wa Israel anapanga njama ili Aziz Duek
Spika wa Bunge la Palestina ahukumiwe adhabu ya kifungo cha miezi 38
jela kwa tuhuma za kutoa matamshi yanayokinzana na sera za utawala huo
ghasibu. Mbunge Khalil Rabi'i ameongeza kuwa, Spika Duek pamoja na
wabunge wengine kadhaa ambao wanashikiliwa kwenye korokoro za Israel
wanakabiliwa na maradhi sugu, amma utawala wa Israel unagoma kutoa
huduma za matibabu na dawa kwa wawakilishi hao wa Palestina. Utawala wa
Kizayuni wa Israel licha ya kukiuka kinga ya wabunge wa Bunge la
Palestina na kuendeleza vitendo vya ukandamizaji dhidi ya viongozi wa
Kipalestina, unawashikilia pia wabunge 36 wakiwemo mawaziri watatu wa
zamani wa Palestina.
0 comments:
Post a Comment