Roketi
ya safari za anga za juu iliyokua ikielekea Kituo cha Kimataifa cha
Anga za juu imelipuka wakati ikiruka kutoka jimbo la Virginia nchini
Marekani.
Roketi Antares, yenye urefu wa ghorofa 14 ikiwa
imetengenezwa na shirika la Orbital Sciences Corp, ililipuka sekunde
chache baada ya kuruka katika kituo cha Wallops Flight Facility.
Chanzo cha tatizo la kulipuka kwa roketi hiyo ya mizigo bado hakijafahamika.
Mipango
ya kurusha roketi hiyo ya anga za juu Jumatatu, ilicheleweshwa kutoka
na boti iliyokuwa karibu na eneo la maji la kurukia roketi hiyo.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwa ya tatu kupewa kandarasi na Shirika la taifa la kusimamia safari za anga za juu la Marekani, NASA.
Roketi
hiyo ilitarajiwa kubeba karibu kilo 2,200 za shehena kwa ajili ya
wanaanga sita walioko katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
"Tutajua
kilichotokea, tunatumaini hivi karibuni, na tutaendelea vizuri na
mipango yetu," amesema Frank Culbertson, makamu-rais mtendaji wa shirika
la Orbital Sciences.
"Wote tumeona hili jambo likitokea kabla
katika shughuli zetu, na wote tumeona kampuni husika zikiimarika
kutokana na tukio kama hili, na tutafanya vivyo hivyo."
Hakuna aliyejeruhiwa, amesema
Bwana Culbertson, na kundi la wataalam wachunguzi tayari walikuwa
wakipitia data kujaribu kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Amesema, Jumatano asubuhi, kazi ya upimaji wa mabaki katika eneo la tukio ingeanza.
Uchunguzi
hautarukia kwenye hitimisho lakini kundi moja la uchunguzi
litajielekeza kuchunguza injini za roketi hiyo AJ-26 zilizotumika
kuinyanyua roketi hiyo kutoka eneo la kurukia, anasema Jonathan Amos,
mwandishi wa BBC wa masuala ya sayansi.
"Kwa kweli hizi ni injini
za Kirusi zilizoboreshwa ambazo kwa asili zilitengenezwa kwa ajili ya
roketi za Urusi za kwenda mwezini za N-1.
"Zilitengenezwa kufikia viwango vya kisasa, lakini moja ililipuka wakati wa majaribio ardhini mapema mwaka huu."
0 comments:
Post a Comment