Wanajeshi katika kambi ya jeshi ya Nyali iliopobmjini Mombasa pwani ya Kenya wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 6 baada ya genge la wahalifu kuvamia kituo hicho cha jeshi mapema leo. Inadaiwa kuwa kundi la watu 15 lilijaribu kuvamiabkambi hiyo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ya jumapili. Wanajeshi waliokuwa katika zamu waliwezabkulidhibiti kundi hilo ambapo watu watano waliuawa huku askari mmoja akiweza kujeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na wavamizi hao. Kufikia sasa maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha shambulizi jilo. Hatahivyo wengi wanashuku watu hao huenda ni
wanachama wa kundi la Mombasa RepublicanbCouncil MRC. Lakini msemaji wa kundi hilo Randu Nzai amekanusha habari hizo akisema kuwa kundi hilo halikuhusika kamwe.
0 comments:
Post a Comment