UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kagera umelalamikia kitendo kinachofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutumia janga la tetemeko la ardhi mjini hapa kufanya siasa na propaganda potofu.
Pia umoja huo umeitaka na kuishauri Serikali kuacha kazi ya uhakiki, ugawaji wa misaada yote kwa waathirika ifanywe na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alimueleza suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu, alipomtembelea ofisini kwake.
Alimweleza kuwa kinachofanywa na Chadema ni kituko na fedheha ya kisiasa. Alisema baadhi ya viongozi wa chama hicho wanatumia tetemeko hilo kujaribu kujijenga kisiasa huku wakiwabagua wanachama wa CCM kwa itikadi za kisiasa.
Alisema uhakiki na utoaji wa msaada katika awamu ya kwanza ulifanyika kukiwa na ubaguzi na upendeleo huku baadhi ya shehena za mizigo ya misaada na vifaa vya ujenzi ikiandikwa maneno “ukawa pamoja”.
0 comments:
Post a Comment