Washtakiwa wa kesi inayowakabili
viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kidini (Jumiki) Zanzibar,
wamesomewa mashtaka mapya katika Mahakama Kuu.
Mwendesha Mashtaka, Ramadhan Nassib aliyasoma mashtaka hayo mapya yanayowakabili mbele ya Jaji Fatma Hamid Mahamoud.
Nassib alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na madai
ya kuharibu mali, uchochezi, ushawishi na kuham asisha fujo na kula
njama ya kufanya kosa.
Mshtakiwa Azan Khalid (48), anakabiliwa na kosa la
ziada peke yake akidaiwa kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha
uvunjifu wa amani.
Alidai makosa yote hayo yalifanyika kati ya Oktoba 17, 18 na 19 maeneo tofauti na washtakiwa wote walikana madai hayo.
Licha ya Azan, washtakiwa wengine ni Masheikh
Farid Hadi (41), Mselem Ali Mselem (52), Mussa Juma Mussa (47), Suleiman
Juma Suleiman (66), Khamis Ali Suleiman (59) na Hassan Bakar Suleiman
(39).
Nassib alidai kuwa upelelezi umekamilika, lakini
aliomba Mahakama kufanya subira ya kutoa uamuzi wowote vile upande wao
umekata rufani Mahakama ya Rufaa na unaweza ukaathiri uamuzi wa Mahakama
hiyo.
Mawakili wa watetezi ukiongozwa na Taufik Salum
uliomba Mahakama hiyo, kuwapatia dhamana washtakiwa hao kwa vile wako
rumande muda mrefu.
Jaji Mahmoud alisema atapitia kwa undani maombi ya pande zote mbili, kwa vile ni mgeni katika kesi hiyo na atatoa uamuzi.
Aliahirisha kesi hiyo hadi kesho.
chanzo mwananchi
0 comments:
Post a Comment