MHE
Kikwete aliwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa
ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo
lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu
leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili
watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa,
wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa
kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia.jengo
lililoporomoka lilikuwa la ghorofa la 15, likijengwa ubavuni mwa
Msikiti wa Shia Ithnaasheri.POLENI SANA TANZANIA. TUSHIKAMANE KUWAFARIJI
WOTE WALIOATHIRIKA NA JANGA HILI
Ni msiba na majonzi ni baada ya kuporomoka kwa jengo
la ghorofa kumi na tano linalomilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la
Nyumba la Taifa NHC na kampuni ya
Aliraza Investiments Ltd ya jijini Dar es salaam huku mjenzi wa jengo
hilo ikiwa ni kampuni ya ujenzi ya Luck Construction Ltd, mpaka sasa
uokoaji unaendelea lakini ukionekana kusuasua kutokana na ufinyu wa eneo
lenyewe na vifaa hafifu vya kuokolea, bado haijafahamika kwamba ni watu
wangapi wamepoteza maisha katika ajali hiyo na wangapi wamejeruhiwa ,
magari ya kubebea wagonjwa yamekuwa yakipishana mara kwa mara wakati
yakipeleka ama majeruhi ama watu waliopoteza maisha katika tukio hilo la
kusikitisha.
tanzania na matukjo ya ajabu mpaka lini jamani!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete