..................................................................................................
Joseph J.Mungai MB (mstf0
P.O.BOX 34 Mafinga
S: 0753 192999
BP: jjmungai@tatepa.com
BARUA YA WAZI KWA TUME YA ELIMU
YA KUFELI 60% MTIHANI WA KVI 2012
ILIYOTEULIWA NA MHE WAZIRI MKUU
29/03/2013
Kumb Na. JJM/2013/ELIMU/19
Kwa Mwenyekiti
Tume ya Elimu ya Kufeli KIV
Ofisi ya Waziri Mkuu
DAR ES SALAAM
Ndugu Mwenyekiti
KUONGEZEKA WANAOFELI KIV KUTOKA 9.7%
MWKA 2007 HADI 60% 2012
1.1
Nnawapongeza
kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau fwa elimu kuwaletea maoni na au/ushauri.
2.0
Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa
Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education Trust (MET) iliyoanzisha katika
wilaya ya Mufindi na
kuziendesha kwa mika zaidi
ya 10 Sekondari 9 za: (1) JJ
Mungai (2) Sadani ( 3) Itengule ( 4)
Igowole ( 5) Itandula ( 6) Mgololo ( 7 ) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo;
ambazo sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na
Utamaduni mwaka 2000 hadi 2005.
3.0 Kabla ya
kutoa ushauri naoba kuipa Tume yako ufahamu
wa ukweli ufuatao:
3.1
Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio
lililoibuka ghafla bali waliofeli ( Division 0) mtihani huo waliongezeka kutoka
mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa
2012:60%!!!!!
3.2
Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka
1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%,
2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi
2007 ni 10%. Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka
2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST ( Basic Statics in
Education, National Data) ya miaka
husika.
3.3
Kati
ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne
walikuwa wastani wa 10% ambayo inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na
2008
kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa
kuonge
zeka kila mwaka
hadi kufikia 60% ya mwaka
huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada
ya matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya “utafiti kudadisi sababu
za ufaulu huo mbaya” na taarifa yake ipo
kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni”,
lakini hadi leo haikusomwa. Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo
kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja
isiyo ya siri ya ndani ya wizara ya Elimu.
4.0
Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo yanaweza kusomwa katika maandiko mawili
ya Wizara ya Elimu yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi
2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa
maboresho hayo uzito w akisheria
yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla
ya wakati wake. Maboresho yamewekwa kando moja baada ya jingine au
hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi ilivyokuwa kabla ya mwaka 2000.
USHAURI:
5.0
Kwa kuwa Elimu ni nyenzo muhimu sana
kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na kucho cchea maendeleo
ya nchi nimeamua kutonyamaza na kuwa muwazi kabisa, ingawaje mimi ni
mwanasiasa niliyestaafu. Kwa hiyo
NASHAURI mambo yafuatayo:
5.1
Utaratibu sahihi wa kupanda madarasa kwa
ufaulu ( achievement based progression)
uliowekwa na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na
uimarishwe bila kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza, la pili na la Tatu ambayo Mwalimu Mkuu siku zote anayo
madaraka ya kukalilisha, kama
mwanafunzi hajazijua “K” 3: kusoma,
kuandika na kuhesabu.
5.2
Tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya
Elimu niliyoyataja akatika 4(a) na (b)
hapo juu yaliyomo maboresho ya elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha
kufaulu vizuri katika Elimu ya Msingi na Sekondari miaka ya 2004-2007; badala ya kutumia muda
mwingi na fedha n=yingi kugundua upya gurudumu.
5.3
Taasisi ya Elimu Tanzania ( Tanzania Institute of
Education –TIE) iagizwe na iachiwe
kutekeleza wajibu wake wa
kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.
5.4
Wanasiasa tuache kuamua bila kuzingatia
ipasavyo utafiti na ushauri w kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.
Kutokana
na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua
hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu imerudi ilikokuwa kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu
limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha
kuingilia na kuamua bila kuzingatia
utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo
mabaya kama hayo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya
mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi
hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia “ anayeficha maradhi kifo kitamuumbua”
Wasalamu
Joseph J Mungai MB mstf
MDAU WA ELIMU
0 comments:
Post a Comment