Muasi Bosco Ntaganda
anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo inadaiwa amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani
mjini Kigali, Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise
Mushikiwabo amesema taarifa walizonazo ni kuwa Kiongozi huyo muasi yuko
chini ya ulinzi wa Marekani katika ubalozi wake."Tumefahamishwa hii leo (Jumatatu) kuwa Bosco Ntaganda ameingia Rwanda na kujisalimisha katika Ubalozi wa marekani hapa Kigali", amesema Louise Mushikiwabo
Jenerali Ntaganda amekanusha mashitaka yanayomkabili katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC kwamba anahusika na uhalifu wa kivita na ule dhidi ya binadamu.
Hata hivyo Marekani haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hizo za kujisalimisha kwa Jeneral huyo muasi katika ubalozini wake.
CHANZO: BBC
0 comments:
Post a Comment