Na Zulfa Mfinanga,Mwananchi
(email the author)
Shinyanga. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
amesema chama chake hakihusiki na mpango wa uchochezi na utekaji
unaodaiwa kufanywa na mwanachama wake, Alfred Lwakatare dhidi ya
mwandishi wa habari Absalom Kibanda.
Kauli hiyo aliitoa mjini Shinyanga alipokuwa
akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Shycom
mjini hapa kuhusu utata wa kukamatwa na kuhojiwa kwa mmoja wa viongozi
wa Chadema.
“Wanasema eti sisi tumemteka Kibanda, kwa sababu
gani, kwa vikosi vipi na kwa silaha zipi, huo mpango wanaujua wao, na
tunasema hatutarudi nyuma, wasifikiri kumkamata mpiganaji wetu
wataififisha nguvu ya Chadema wanajidanganya” , aisema Mbowe.
Mbowe pia alisisitiza kauli yake ya kuitisha
maandamano nchi nzima ya kumshinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha
nne mwaka huu kwamba yatafanyika.
Alisema maandamano hayo yamepangwa kuwa siku ya Mei 15, mwaka huu.
Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano ya
wanachama wa chama hicho na viongozi wao baada ya mkutano mkuu wa Mikoa
ya Shinyanga, Simiyu na MaraAwali mbunge wa Jimbo Maswa Mashariki,
Sylvester Kasulumbayi aliwataka wakulima wa pamba kutokipigia kura CCM
kwa maelezo kwamba kimewaingiza katika dimbwi la umaskini kwa kushindwa
kusimamia bei ya zao la pamba.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment